Matthew 22:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakamwambia, “Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwalimu, Musa alisema, ‘Mtu akifa bila kuwa na watoto, ndugu yake inampasa amwoe huyo mjane ili ampatie watoto huyo nduguye aliyekufa.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakasema, “Mwalimu, Musa alituambia kuwa ikiwa mwanaume aliyeoa atakufa na hana watoto, ndugu yake lazima amwoe mkewe ili aweze kuzaa watoto kwa ajili ya nduguye aliyekufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wakamwambia, “Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, amzalie ndugu yake watoto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakamwambia, “Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwalimu, Mose alisema, ‘Kama mtu akifa bila kuwa na watoto, ndugu yake amwoe huyo mjane ili ampatie watoto huyo nduguye aliyekufa.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwalimu, Musa alisema, ‘Kama mtu akifa bila kuwa na watoto, ndugu yake inampasa amwoe huyo mjane ili ampatie watoto huyo nduguye aliyekufa.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakamwambia, “Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakisema: Mfunzi, Mose alisema: Mtu akifa asipokuwa na wana, nduguye amwingilie mkewe, amzalie mkubwa wake mwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamwuliza: “Mwalimu, Musa alisema: ‘Mutu akikufa bila kuacha mutoto, ndugu yake anapaswa kumwoa yule mujane na kumuzalia marehemu watoto.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakinena, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, nae hana watoto, ndugu yake amwoe mkewe, illi ampatie ndugu yake mzao.