Matthew 22:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa: Karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ndama wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari; njoni harusini.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kisha akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa kwamba nimeandaa chakula. Nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono, karamu iko tayari. Karibuni kwa karamu ya arusi.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng'ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo mfalme aliwaita baadhi ya watumishi wengine zaidi na akawaambia namna ya kuwaambia wale aliowaalika: ‘Njooni sasa! Sherehe imeandaliwa. Nimechinja ng'ombe wangu madume na ndama wanono waliolishwa nafaka, na kila kitu kiko tayari kuliwa. Njooni kwenye sherehe ya harusi.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa: karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ng'ombe wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari, njoni arusini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa: karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ndama wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari; njoni harusini.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kisha akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa kwamba karamu iko tayari kwa ajili yenu, nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono. Karibuni.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kisha akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa kwamba nimeandaa chakula. Nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono, karamu iko tayari. Karibuni kwa karamu ya arusi.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng'ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni harusini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa: Karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ndama wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari; njoni harusini.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akatuma watumwa wengine akisema: Waambieni walioalikwa: Tazameni, nimekwisha kuiandaa karamu yangu, ng'ombe na vinono vimechinjwa, vyote viko tayari, njoni arusini!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng’ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akawatuma watumishi wengine, akisema: ‘Mwende kuwaambia waalikwa kwamba karamu yangu iko sasa tayari. Nimechinja ngombe na nyama wenye kunona; vitu vyote viko tayari. Muwaambie wafike kwa karamu!’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akatuma tena watumishi wengine, akinena, Waambieni wale walioalikwa, Tʼazameni nimeandaa karamu yangu: ngʼombe na vinono vimekwisha kuehinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini.