Matthew 22:46 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakuna mtu aliyeweza kumjibu Isa neno. Tena tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu kumuuliza tena maswali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakuna Farisayo aliyeweza kumjibu Yesu. Na baada ya siku hiyo, hakuna aliyekuwa jasiri kumwuliza maswali zaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakuna mtu aliyeweza kumjibu Yesu neno. Tena tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu kumwuliza tena maswali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakuna mtu aliyeweza kumjibu Isa neno. Tena tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu kumuuliza tena maswali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu yeyote tangu siku ile kumwuliza neno tena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata mmoja hakuweza kumjibu neno, wala toka siku ile hakuwako mtu aliyejipa moyo wa kumwuliza neno tena.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi hakuna mutu aliyeweza kumujibu neno, na tangia siku ile hakuna aliyesubutu kumwuliza tena neno.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu tangu siku ile kumwuliza neno tena.