Matthew 22:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake wakawaangamize wauaji hao na kuuteketeza mji wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mfalme akakasirika sana, akapeleka jeshi lake likawaangamiza wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi yule mfalme akaghadhibika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mfalme alikasirika sana na akatuma jeshi lake kuwaua wale waliowaua watumwa wake. Na jeshi likauchoma moto mji wao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake wakawaangamize wauaji hao na kuuteketeza mji wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake wakawaangamize wauaji hao na kuuteketeza mji wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mfalme akakasirika sana, akapeleka jeshi lake likawaangamiza wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mfalme akakasirika sana, akapeleka jeshi lake likawaangamiza wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi yule mfalme akaghadhibika; akatuma majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake wakawaangamize wauaji hao na kuuteketeza mji wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mfalme akachafuka, akawatuma askari wake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi yule mfalme akaghadhibika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu mufalme akakasirika. Akawatuma waaskari wake kuwaua wale wauaji na kuteketeza muji wao kwa moto.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi yule mfalme alipopata khahari, akaghadhabika: akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.