Matthew 23:14 — Compare Translations
12 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnawanyonya wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali.] (Taz Marko 12:40).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ole wenu walimu wa Torati na Mafarisayo, enyi wanafiki! Mnakula katika nyumba za wajane, nanyi kwa kujifanya kuwa wema, mnasali sala ndefu. Kwa hiyo hukumu yenu itakuwa kuu zaidi.]
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
[Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.]
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnawanyonya wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, enyi wanafiki! Mnakula katika nyumba za wajane, nanyi kwa kujifanya kuwa wema, mnasali sala ndefu. Kwa hiyo adhabu yenu itakuwa kubwa zaidi.]
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ole wenu walimu wa Torati na Mafarisayo, enyi wanafiki! Mnakula katika nyumba za wajane, nanyi kwa kujifanya kuwa wema, mnasali sala ndefu. Kwa hiyo hukumu yenu itakuwa kuu zaidi.]
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
[Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.]
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnawanyonya wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali.] (Taz Marko 12:40).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani mnazila nyumba za wajane mkijitendekeza, kama mnakaza kuwaombea. Kwa hiyo mapatilizo yenu yatakuwa kuliko ya wengine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
[Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.]
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ole kwenu, ninyi walimu wa Sheria na Wafarisayo, ninyi wanafiki! Munanyanganya mali za wajane na kuomba maombi marefu kwa kujionyesha. Kwa sababu hii azabu yenu itakuwa kubwa zaidi!]
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, nao wanaoingia hamwaachi waingie.