Matthew 23:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena mwasema ati mtu akiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapa kwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu, kiapo hicho humshika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia mnasema, ‘Mtu akiapa kwa madhabahu, si kitu; lakini mtu akiapa kwa sadaka iliyo juu ya madhabahu, amefungwa kwa kiapo chake’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na mnasema, ‘Mtu yeyote akitumia madhabahu kuweka nadhiri au kiapo, haina maana yeyote. Lakini kila anayetumia sadaka iliyo kwenye madhabahu na kuapa au kuweka nadhiri, lazima atimize nadhiri au kiapo hicho.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena mwasema ati mtu akiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapa kwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu, kiapo hicho humshika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena mwasema ati mtu akiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapa kwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu, kiapo hicho humshika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia mnasema, ‘Mtu akiapa kwa madhabahu, si kitu, lakini mtu akiapa kwa sadaka iliyo juu ya madhabahu, amefungwa kwa kiapo chake’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia mnasema, ‘Mtu akiapa kwa madhabahu, si kitu; lakini mtu akiapa kwa sadaka iliyo juu ya madhabahu, amefungwa kwa kiapo chake’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga kwa kiapo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena mwasema ati mtu akiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapa kwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu, kiapo hicho humshika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mnasema: Mtu atakapoapa na kuitaja meza ya Bwana, si kitu; lakini atakapoapa na kukitaja kipaji kilichoko juu yake amejifunga!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munasema vilevile kwamba mutu akiapa akitaja mazabahu, si kitu; lakini kama akiapa akitaja sadaka inayokuwa juu yake, anapaswa kutimiza kiapo chake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena, Mtu atakaeapa kwa madhbahu, si kitu; bali mtu atakaeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga.