Matthew 23:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyanganyi na uchoyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ole wenu, walimu wa Torati na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ole wenu walimu wa sheria nanyi Mafarisayo! Ninyi ni wanafiki! Mnaosha vikombe na sahani zenu kwa nje. Lakini ndani yake vimejaa vitu mlivyopata kwa kuwadang'anya wengine na kujifurahisha ninyi wenyewe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyang'anyi na uchoyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyang'anyi na uchoyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnasafisha nje ya kikombe na kisahani, lakini ndani mmejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ole wenu, walimu wa Torati na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyanganyi na uchoyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani vinyweo na vyano mnaviosha nje, lakini ndani vimejaa mapokonyo na mapujufu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ole kwenu, ninyi walimu wa Sheria na Wafarisayo, ninyi wanafiki! Ninyi ni kama mutu anayesafisha tu inje ya kikombe na sahani, lakini ndani kumejaa vitu mulivyovipata kwa njia ya wizi na tamaa mbaya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa nmasafisha nje ya kikombe na chungu, na ndani yake vimejaa unyangʼanyi na kutoa kuwa na kiasi.