Matthew 23:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa safi pia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ewe Farisayo kipofu! Safisha ndani ya kikombe na sahani kwanza, ndipo nje itakuwa safi pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mafarisayo, ninyi ni wasiyeona! Safisheni kwanza vikombe kwa ndani ili viwe safi. Ndipo vikombe hivyo vitakuwa safi hata kwa nje.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa safi pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa safi pia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Enyi Mafarisayo vipofu! Safisheni kwanza ndani ya kikombe na kisahani, ndipo nje patakuwa safi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ewe Farisayo kipofu! Safisha ndani ya kikombe na sahani kwanza, ndipo nje itakuwa safi pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nako kupate kuwa safi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa safi pia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Fariseo kipofu, kwanza osha ndani yake kinyweo na chano, vipate kuwa safi hata nje!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe kipofu Mufarisayo! Safisha kwanza ndani ya kikombe na ya sahani, na kisha inje yake kutakuwa safi vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ewe Farisayo kipofu, takasa kwanza ndani ya kikombe na chungu, illi nje yake nayo ipate kuwa safi.