Matthew 23:34 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndio maana mimi ninawapelekea nyinyi manabii, watu wenye hekima na waalimu; mtawaua na kuwasulubisha baadhi yao, na wengine mtawapiga viboko katika masunagogi yenu na kuwasaka katika kila mji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu hii, tazameni, natuma kwenu manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwasulubisha, na wengine wao mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na kuwafuatia kutoka mji mmoja hadi mji mwingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo ninawaambia: Ninawatuma manabii na walimu wenye hekima na wanaojua Maandiko. Lakini mtawaua, mtawatundika baadhi yao kwenye misalaba na kuwapiga wengine katika masinagogi yenu. Mtawafukuza kutoka katika mji mmoja hadi mwingine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndiyo maana mimi ninawapelekea ninyi manabii, watu wenye hekima na walimu; mtawaua na kuwasulubisha baadhi yao, na wengine mtawapiga viboko katika masunagogi yenu na kuwasaka katika kila mji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndio maana mimi ninawapelekea nyinyi manabii, watu wenye hekima na waalimu; mtawaua na kuwasulubisha baadhi yao, na wengine mtawapiga viboko katika masunagogi yenu na kuwasaka katika kila mji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu hii tazama nawapelekea manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwasulibisha, wengine mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na wengine mtawafuatia kutoka mji mmoja hadi mji mwingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu hii, tazameni, natuma kwenu manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwasulubisha, na wengine wao mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na kuwafuatia kutoka mji mmoja hadi mji mwingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulubisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndio maana mimi ninawapelekea nyinyi manabii, watu wenye hekima na waalimu; mtawaua na kuwasulubisha baadhi yao, na wengine mtawapiga viboko katika masunagogi yenu na kuwasaka katika kila mji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Kwa sababu hii tazameni, mimi natuma kwenu wafumbuaji na werevu wa kweli na waandishi; wengine wao mtawaua na kuwawamba misalabani, wengine wao mtawapiga katika nyumba zenu za kuombea, kisha mtawafukuza mji kwa mji;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu hiyo, nitawatumia manabii na watu wenye hekima na walimu. Mutawaua wamoja wao, mutatundika wengine juu ya misalaba, mutawapiga wengine fimbo ndani ya nyumba zenu za kuabudia na kuwafukuza muji kwa muji.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu hii, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi: na wengine wao mtawaua na mtawasulibi, na wengine wao mtawapiga katika sunagogi zenu, na mtawafukuza mji kwa mji;