Matthew 23:37 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Yerusalemu! Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya watoto wako kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ee Yerusalemu, Yerusalemu! Unayewaua manabii. Unawapiga kwa mawe wale ambao Mungu amewatuma kwako. Mara nyingi nimetaka kuwasaidia watu wako. Nimetaka kuwakusanya watu wako kama kuku anavyowakusanya vifaranga wake chini ya mbawa zake. Lakini hukuniruhusu kufanya hivyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Yerusalemu, Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya watoto wako kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Yerusalemu! Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya watoto wako kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ee Yerusalemu, mnaowaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwenu! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku awakusanyavyo pamoja vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Yerusalemu! Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya watoto wako kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yerusalemu, Yerusalemu, unawaua wafumbuaji, ukawapiga mawe walitumwa kwako! Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako, kama kuku anavyovikusanya vifaranga vyake mabawani! Lakini hamkutaka!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ewe Yerusalema, Ewe Yerusalema. Wewe unaua manabii na kuwatupia mawe wale ambao Mungu anakutumia. Mara nyingi nilitaka kuwakusanya wakaaji wako kama vile kuku anavyokusanya vitoto vyake chini ya mabawa yake, lakini ninyi hamukutaka!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ee Yerusalemi, Yerusalemi, wenye kuwaua manabii, na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkukubali!