Matthew 23:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye maandishi ya sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za makoti yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wao wanatenda mambo mema tu ili waonwe na watu wengine. Hufanya visanduku vidogo vya Maandiko wanavyovaa kuwa vikubwa zaidi. Hufanya mashada ya urembo kwenye mavazi yao ya nje kuwa marefu zaidi ili waonwe na watu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye maandishi ya Sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za makoti yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye maandishi ya sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za makoti yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hufanya vikasha vya ngozi vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye maandishi ya sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za makoti yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Matendo yao yote huyafanyia kutazamwa na watu. Hukuza makaratasi ya kuombea, huviongeza navyo vishada vya nguo zao, viwe vinene.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafanya matendo yao yote tu kusudi wajionyeshe mbele ya watu. Wanajifungia kwa paji za nyuso vibweta vipana vyenye vikaratasi vya Maandiko Matakatifu. Nao wanavaa kanzu zenye pembe ndefu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena matendo yao yote huyatenda illi kutazamwa na watu: hupanua fulakteria zao, huongeza matamvna ya mavazi yao;