Matthew 24:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Injili hii ya ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na Habari Njema niliyoihubiri kuhusu Ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote. Itatawanywa katika kila taifa. Kisha mwisho utakuja.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya Ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni pote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo ule mwisho utakapokuja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Habari Njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao huu utume mwema wa ufalme wa Mungu utatangawa ulimwenguni mote, uje, unishuhudie kwa wamizimu wote. Kisha ndipo, mwisho utakapokuja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na hii Habari Njema ya Ufalme itahubiriwa katika dunia nzima kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; na halafu mwisho wa dunia utatimia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na injili hii ya ufalme itakhubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; ndipo ule mwisho utakapokuja.