Matthew 24:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi, mtakapoona ‘Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake),
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu),
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nabii Danieli alizungumza kuhusu ‘jambo la kutisha litakalosababisha uharibifu.’ Mtakapoliona jambo hili la kutisha limesimama patakatifu.” (Asomaye hili anapaswa kuelewa jambo hili linamaanisha nini.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Basi, mtakapoona Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake),
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi, mtakapoona ‘Chukizo Haribifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake),
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, asomaye na afahamu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu),
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Basi, mtakapoona ‘Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake),
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Hapo ndipo, mtakapochafukwa mioyo mkiona, mwangamizaji atapishaye akisimama mahali Patakatifu, kama mfumbuaji Danieli alivyosema; mwenye kupasoma hapa sharti aangalie, ajue maana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mutamwona yeye anayeitwa ‘Chukizo Linaloleta Uharibifu,’ yule aliyetajwa na nabii Danieli, akisimamishwa katika hekalu. (Anayesoma maneno haya aelewe maana yake.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi mlionapo chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama mahali patakatifu (asomae afahamu),