Matthew 24:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, wala haitapata kutokea tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwepo tangu mwanzo wa dunia hadi sasa: wala haitakuwepo tena kamwe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
kwa sababu utakuwa wakati wa dhiki kuu. Kutakuwepo na usumbufu mwingi sana kuliko ule uliowahi kutokea tangu mwanzo wa ulimwengu. Na hakuna jambo baya kama hilo litakalotokea tena.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, wala haitapata kutokea tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, wala haitapata kutokea tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa, wala haitakuwako tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa: wala haitakuwako tena kamwe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, wala haitapata kutokea tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hapo patakuwa na maumivu makuu kuyapita yote yaliyopatikana tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka sasa, hata halafu hayatapatikana tena kama hayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana katika siku zile kutakuwa mateso makubwa yasiyotokea tangia kuumbwa kwa dunia mpaka sasa, wala hakutatokea tena mateso kama yale.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana wakati ule itakuwapo shidda kubwa, jinsi isivyopata kuwa tangu mwanzo wa ulimweugu hatta leo, wala haitakuwa kamwe.