Matthew 24:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna mtu ambaye angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, siku hizo zitafupishwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Mungu amekwisha amua kuufupisha wakati huo. Ikiwa usingefupishwa, hakuna ambaye angeendelea kuishi. Lakini Mungu ataufupisha ili kuwasaidia watu aliowachagua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama siku hizo zisingelifupizwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeliokoka, lakini kwa ajili ya wateule siku hizo zitafupizwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, siku hizo zitafupizwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama siku hizo zisingalifupishwa, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule siku hizo zitafupishwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo siku zile kama hazingalipuinguzwa, hangaliokoka mtu hata mmoja. Lakini kwa ajili ya wale waliochaguliwa siku zile zitapunguzwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kama Mungu asingepunguza siku zile za mateso, hakuna hata mutu mumoja angeponyoka kufa. Lakini kwa ajili ya watu wake aliowachagua, yeye atazipunguza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kama siku zile zisingalikatizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitakatizwa siku zile.