Matthew 24:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana watatokea akina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana watatokea masihi wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara kubwa na maajabu mengi ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule hasa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Manabii wa uongo na masihi wa uongo watatokea na kufanya miujiza na maajabu makuu, ili ikiwezekana wawadanganye wateule.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana watatokea akina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo na kufanya ishara kubwa na miujiza mingi ili kuwapotosha, hata ikiwezekana wale wateule hasa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana watatokea masihi wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara kubwa na maajabu mengi ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule hasa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana watatokea Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, ikiwezekana, hata walio wateule.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana watatokea akina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani watainuka makristo wa uwongo na wafumbuaji wa uwongo; nao watatoa vielekezo vikubwa na vioja, wawapoteza hata waliochaguliwa, kama inawezekana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwa maana kutatokea watu wanaojiita kwa uongo ‘Kristo’ pamoja na manabii wa uongo, nao wataonyesha vitambulisho vikubwa na maajabu, hata ikiwezekana, wawadanganye hata watu waliochaguliwa na Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.