Matthew 24:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa mavuno umekaribia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Jifunze kwa mtini: Matawi yake yanapokuwa ya kijani na laini na kuanza kutoa majani mapya, ndipo mnatambua kuwa majira ya joto yamekaribia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa mavuno umekaribia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Jifunzeni kutokana na mtini. Matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchipua majani, fahamuni kwamba kiangazi kimekaribia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mnatambua ya kuwa wakati wa mavuno uko karibu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa mavuno umekaribia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jifundisheni mfano kwa mkuyu: matawi yake yanapochipua na kuchanua majani, mnatambua, ya kuwa siku za vuli ziko karibu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Muangalilie mufano juu ya muti wa tini. Wakati matawi yake yanapochipuka, nayo majani yao yanapochipuka, ninyi munatambua kwamba wakati wa jua kali unakaribia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa mtini jifunzeni mfano: tawi lake likiisha kuwa laini na kuchanua majani, mwafahamu ya kuwa wakati wa hari ni karibu;