Matthew 24:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo haya yote yakitendeka, jueni kwamba yuko karibu sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo, mnapoyaona mambo haya yote, mtambue kwamba wakati u karibu, hata malangoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika namna hiyo hiyo, mtakapoona mambo haya yote yakitokea, mtajua kuwa wakati umekaribia wa kile kitakachotokea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo haya yote yakitendeka, jueni kwamba yuko karibu sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo haya yote yakitendeka, jueni kwamba yuko karibu sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, mwonapo mambo hayo, jueni kwamba yu karibu malangoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yote, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nanyi kadhalika, myaonapo mambo hayo yote, tambueni ya kuwa yuko karibu, katika malango.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo haya yote yakitendeka, jueni kwamba yuko karibu sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vivyo hivyo nanyi mtakapoyaona hayo yote tambueni, ya kuwa mwisho umewafikia milangoni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile, wakati mutakapoona mambo haya yote niliyotoka kutaja yanatokea, mujue kwamba yeye yuko karibu, na amekuwa kwa mulango.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
vivyo hivyo na ninyi, myaonapo haya yote, fahamuni ya kuwa yu karibu, tena milangoni.