Matthew 24:36 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa habari ya siku ile na saa, hakuna ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakuna anayeijua siku wala wakati. Malaika wa mbinguni hawaijui hata Mwana hajui itakuwa lini. Baba peke yake ndiye anayejua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake ndiye ajuaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa habari ya siku ile na saa hakuna ajuaye, hata malaika mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa habari ya siku ile na saa, hakuna ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kuhusu siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ile siku na saa yake itakapofikia, mtu hapajui, wala malaika wa mbingu, wala Mwana, ila Baba peke yake tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Lakini hakuna mutu anayejua siku ile na saa, hata wamalaika wa mbinguni, hata Mwana, isipokuwa Baba peke yake tu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na khabari ya siku ile na saa ile hakuna ajuae, hatta malaika walio mbinguni, illa, Baba yangu peke yake.