Matthew 24:43 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kumbukeni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua ni wakati gani wa usiku ambao mwizi atakuja, angekesha na hangekubali nyumba yake kuvunjwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwenye nyumba angefanya nini ikiwa angejua wakati ambao mwizi atakuja? Mnajua angelikesha ili mwizi asivunje na kuingia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini kumbukeni jambo hili: kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kumbukeni jambo hili: kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini fahamuni hili kwamba: Kama mwenye nyumba angelijua ni wakati gani wa usiku ambao mwivi anakuja, angelikesha na asingeliiacha nyumba yake kuvunjwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua ni wakati gani wa usiku ambao mwizi atakuja, angekesha na hangekubali nyumba yake kuvunjwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliujua ule wakati mwizi atakaokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kumbukeni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini litambueni neno hili: Kama mwenye nyumba angaliijua zamu, mwizi atakayojia, angalikesha, asiache, nyumba yake ibomolewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munajua vema kwamba mwenye nyumba angalijua wakati gani mwizi atakapokuja kuiba, angalikesha na kuchunga nyumba yake isibomolewe.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angalijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa.