Matthew 24:45 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akaendelea kusema, “Ni nani basi mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watu wake, awape chakula kwa wakati wake?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Fikiria mtumishi aliyewekwa na bwana wake kuwapa chakula watumishi wake wengine katika muda uliopangwa. Ni kwa namna gani mtumishi huyo atajionyesha kuwa ni mwangalifu na mwaminifu?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akaendelea kusema, “Ni nani basi mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watu wake, awape chakula kwa wakati wake?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akaendelea kusema, “Ni nani basi mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watu wake, awape chakula kwa wakati wake?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati muafaka?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akaendelea kusema, “Ni nani basi mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watu wake, awape chakula kwa wakati wake?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, yuko nani aliye mtumwa mwelekevu na mwerevu, bwana wake akimpa kuwatunza wa nyumbani mwake, awape vyakula, saa yao itakapofika?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Basi ni nani anayekuwa mutumishi mwaminifu na mwenye akili? Ni yule bwana wake aliyemuweka kuwa musimamizi wa watumishi wake wengine na kumwamuru kuwapatia posho yao kwa wakati uliopangwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nani bassi aliye mtumishi yule amini mwenye haki, ambae bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape chakula kwa saa yake?