Matthew 24:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtasikia habari za vita na tetesi za vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtasikia kuhusu vita vinanavyopiganwa na pia matetesi ya kuwapo vita vingine. Lakini msiogope. Mambo haya lazima yatokee na mwisho wenyewe hautafuata palepale.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita, angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mtasikia habari za vita na tetesi za vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mtasikia vita na mavumi ya vita; vitazameni tu, msivihangaikie! Kwani hivyo sharti viwepo, lakini huo sio mwisho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutasikia habari za matokeo au utetezi wa vita, lakini musiogope. Sherti mambo hayo yatukie, lakini hayaonyeshi kama mwisho umefika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mtasikia khabari za vita na uvumi wa vita: angalieni, msitishwe: maana haya hayana buddi kuwa; lakini mwisho wenyewe hado.