Matthew 24:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha mtakamatwa na kupelekwa kwa wenye mamlaka ili mhukumiwe na kuuawa. Watu wote katika ulimwengu watawachukia kwa sababu mnaniamini mimi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa ajili ya jina langu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo watatoa ninyi, mpate kuumizwa, hata kuuawa, tena mtachukiwa na makabila yote kwa ajili ya Jina langu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Halafu watu watawatoa kusudi muteswe na kuuawa, na watu wa mataifa yote watawachukia ninyi kwa ajili yangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakati huo watawasaliti ninyi mpate kuteswa, na watawaua; na mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa vote kwa ajili ya jina langu.