Matthew 25:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana wake akamwambia, ‘Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Bwana wake akajibu, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Bwana wake akajibu, ‘Ulifanya vyema. Wewe ni mtumishi mwema unayeweza kuaminiwa. Ulifanya vizuri kwa kiasi kidogo hicho cha pesa. Hivyo nitakufanya kuwa msimamizi wa mambo makuu. Njoo usherehekee pamoja nami.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana wake akamwambia, ‘Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Bwana wake akajibu, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu, umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache, nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Bwana wake akajibu, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bwana wake akamwambia, ‘Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana wake akamwambia: Vema, wewe mtumwa mwema na mwelekevu, ulikuwa mwelekevu wa machache, nitakupa kutunza mengi. Ingia penye furaha ya bwana wako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana wake akamwambia: ‘Ni vizuri, wewe mutumishi mwema na mwaminifu. Ulikuwa mwaminifu katika ulinzi wa mali ndogo, basi nitakuweka kuwa mulinzi wa mali mingi. Kuja ufurahi pamoja na bwana wako!’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako.