Matthew 25:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Bwana wake akamwambia, ‘Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! Unajua kuwa mimi huvuna mahali ambapo sikupanda, na hukusanya pale ambapo sikutawanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Bwana wake akajibu, ‘Wewe mtumishi mwovu na mvivu! Ulijua kwamba ninavuna mahali nisipopanda na kukusanya mahali nisipotawanya mbegu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Bwana wao akamjibu, ‘Wewe ni mtumishi mbaya na mvivu! Unasema kwamba ulijua ninavuna nisichopanda na ninakusanya mazao ambayo sikupanda mbegu yo yote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Bwana wake akamwambia, Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! Unajua kuwa mimi huvuna mahali ambapo sikupanda, na hukusanya pale ambapo sikutawanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Bwana wake akamwambia, ‘Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! Unajua kuwa mimi huvuna mahali ambapo sikupanda, na hukusanya pale ambapo sikutawanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Bwana wake akajibu, ‘Wewe mtumishi mwovu na mvivu! Ulijua kwamba ninavuna mahali nisipopanda na kukusanya mahali nisipotawanya mbegu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Bwana wake akajibu, ‘Wewe mtumishi mwovu na mvivu! Ulijua kwamba ninavuna mahali nisipopanda na kukusanya mahali nisipotawanya mbegu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Bwana wake akamwambia, ‘Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! Unajua kuwa mimi huvuna mahali ambapo sikupanda, na hukusanya pale ambapo sikutawanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini bwana wake akajibu akimwambia: Mtumwa mbaya wewe! U mvivu! Ulinijua, ya kuwa navuna, nisipopanda, nakusanya nisipotandaza?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye bwana wake akamujibu: ‘Wewe mutumishi mubaya na muvivu! Ulijua kama ninavuna nafasi nisipopanda, na kukusanya nafasi nisiposambaza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bwana wake akajibu, akamwambia, Mtumishi mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;