Matthew 25:29 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila aliyezalisha faida atapata zaidi. Atakuwa na vingi kuzidi mahitaji yake. Lakini wale wasiotumia walivyonavyo kuleta faida watanyang'anywa kila kitu.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana kila mtu mwenye kitu ataongezewa, naye atakuwa navyo tele. Lakini kwa mtu yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kila mwenye mali atapewa, ziwe nyingi zaidi; lakini asiye na kitu atachukuliwa hata kile, alicho nacho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana mutu anayekuwa na kitu ataongezewa kingine; lakini mutu asiyekuwa na kitu, ataondolewa hata kidogo anachokuwa nacho.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana killa aliye na mali atapewa, na kuongezewa: nae asiye nayo, hatta ile aliyo nayo atanyangʼanywa.