Matthew 25:41 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha mfalme atawaambia walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu. Mungu amekwisha amua kuwa mtaadhibiwa. Nendeni katika moto uwakao milele, moto ulioandaliwa kwa ajili ya yule Mwovu na malaika zake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, Ondokeni mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha atawaambia na wale walioko katika mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha atawaambia walioko kushotoni: Ondokeni kwangu, mlioapizwa, mwingie kwenye moto usiozimika, uliowashiwa Satani na malaika zake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kisha mufalme atawaambia wale wanaokuwa kwa upande wake wa kushoto: ‘Muondoke hapa karibu nami, ninyi muliolaaniwa! Muende katika moto usiozimika hata milele, uliotayarishwa kwa ajili ya Shetani na wamalaika wake!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake: