Matthew 25:45 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye atawajibu, ‘Nawaambieni kweli, kila mlipokataa kumtendea mambo haya mmojawapo wa hawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Naye atawajibu, ‘Amin nawaambia, kwa jinsi hamkumtendea mmoja wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkunitendea mimi.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mfalme atajibu, ‘Ukweli ni kuwa, chochote mlichokataa kumfanyia mmojawapo wa watu wangu hapa, hata wale walioonekana kuwa si wa muhimu, mlikataa kunifanyia mimi.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye atawajibu, Nawaambieni kweli, kila mlipokataa kumtendea mambo haya mmojawapo wa hawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye atawajibu, ‘Nawaambieni kweli, kila mlipokataa kumtendea mambo haya mmojawapo wa hawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Naye atawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, kwa jinsi ambavyo hamkumtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkunitendea mimi.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Naye atawajibu, ‘Amin nawaambia, kwa jinsi ambavyo hamkumtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkunitendea mimi.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye atawajibu, ‘Nawaambieni kweli, kila mlipokataa kumtendea mambo haya mmojawapo wa hawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo atawajibu akisema: Kweli nawaambiani: Yote, msiyomtendea mwenzao mmoja tu wa hawa ndugu zangu wadogo, basi hamkunitendea hata mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye mufalme atawajibu: ‘Kweli ninawaambia: kila kitu mulichokosa kumutendea mumoja wa hawa wanaohesabiwa kuwa wadogo, hamukunitendea mimi.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae atawajibu, akinena, Amin, nawaambieni, Kadiri msivyomtendea mmojawapo katika hawo walio wadogo, na mimi hamkunitendea.