Matthew 26:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawaambieni kweli, popote ulimwenguni ambapo hii Habari Njema itahubiriwa, kitendo hiki alichofanya mama huyu kitatajwa kwa kumkumbuka yeye.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo hii Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu lake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Habari Njema itahubiriwa kwa watu wote ulimwenguni. Na ninaweza kuwathibitishia kuwa kila mahali ambako Habari Njema zitahubiriwa, jambo alilofanya mwanamke huyu litahubiriwa pia, na watu watamkumbuka.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nawaambieni kweli, popote ambapo hii Habari Njema itahubiriwa ulimwenguni, kitendo hiki alichofanya mama huyu kitatajwa kwa kumkumbuka yeye.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawaambieni kweli, popote ulimwenguni ambapo hii Habari Njema itahubiriwa, kitendo hiki alichofanya mama huyu kitatajwa kwa kumkumbuka yeye.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninawaambia kweli, mahali po pote habari njema itakapohubiriwa ulimwenguni mwote, jambo hili alilofanya litatajwa pia, kwa ukumbusho wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo hii Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawaambieni kweli, popote ulimwenguni ambapo hii Habari Njema itahubiriwa, kitendo hiki alichofanya mama huyu kitatajwa kwa kumkumbuka yeye.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli nawaambiani: Po pote katika ulimwengu wote, patakapotangazwa Utume huu mwema, patasemwa nacho hiki, alichokitenda yeye, naye akumbukwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kweli ninawaambia: kwa ajili ya kukumbuka mwanamuke huyu, tendo lile alilofanya litaelezwa popote Habari Njema hii itakapohubiriwa katika dunia nzima.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Amin, nawaambieni, Killa ikhuhiriwapo injili hii katika ulimwengu wote, na hilo alilolitenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.