Matthew 26:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya kwanza kabla ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, “Unataka tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimjia Isa wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Ni wapi utakapo tukuandalie uile Pasaka?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ilipofika siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wafuasi wake walimjia Yesu na kumwambia, “Tutaandaa kila kitu kwa ajili yako ili ule mlo wa Pasaka. Unataka tuandae wapi mlo wa Pasaka?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku ya kwanza kabla ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, “Unataka tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya kwanza kabla ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, “Unataka tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu wanafunzi walimjia Yesu wakamwuliza, “Unataka tuandae wapi kwa ajili yako ili kuila Pasaka?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimjia Isa wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Ni wapi utakapo tukuandalie uile Pasaka?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya kwanza kabla ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, “Unataka tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya kwanza ya kula mikate isiyotiwa chachu wanafunzi wakamjia Yesu wakisema: Unataka, tukuandalie wapi, uile kondoo ya Pasaka?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Ni wapi utakapo tukuandalie uile Pasaka?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya kwanza ya karamu ya sikukuu ya Mukate Usiotiwa Chachu, wanafunzi wakamwendea Yesu na kumwuliza: “Ni wapi unapotaka tukutayarishie karamu ya Pasaka?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Wapi unataka tukuandalie uile pasaka?