Matthew 26:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye akawajibu, “Nendeni mjini kwa mwanamume fulani, mkamwambie: ‘Mwalimu anasema, wakati wangu umefika; kwako nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akajibu, “Nendeni kwa mtu fulani huko mjini, mkamwambie, ‘Mwalimu asema hivi: Saa yangu imekaribia. Nitaiadhimisha Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Enendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu asema, Majira yangu ni karibu; kwako nitafanya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akajibu, “Nendeni mjini kwa mtu ninayemfahamu. Mwambieni kuwa Mwalimu anasema, ‘Muda uliowekwa kwa ajili yangu umekaribia sana. Mimi na wafuasi wangu tutakula mlo wa Pasaka katika nyumba yako.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye akawajibu, “Nendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie: Mwalimu anasema, wakati wangu umefika; kwako nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye akawajibu, “Nendeni mjini kwa mwanamume fulani, mkamwambie: ‘Mwalimu anasema, wakati wangu umefika; kwako nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akajibu, “Nendeni kwa mtu fulani huko mjini mkamwambie, ‘Mwalimu asema hivi: Saa yangu imekaribia, nitaiadhimisha Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akajibu, “Nendeni kwa mtu fulani huko mjini, mkamwambie, ‘Mwalimu asema hivi: Saa yangu imekaribia. Nitaiadhimisha Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Nendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu asema, Majira yangu ni karibu; kwako nitafanya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye akawajibu, “Nendeni mjini kwa mwanamume fulani, mkamwambie: ‘Mwalimu anasema, wakati wangu umefika; kwako nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akasema: Nendeni mjini kwa fulani, mmwambie: Mfunzi anasema: Siku zangu zinatimia! Kwako nitaila kondoo ya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Enendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu asema, Majira yangu ni karibu; kwako nitafanya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawaambia kwamba waende katika muji kwa mutu mumoja na kumwambia: “Mwalimu anasema: ‘Siku yangu inakaribia. Mimi na wanafunzi wangu tutakula karamu ya Pasaka kwako.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasema, Enendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu anena, Majira yaugu i karibu; kwako nitafanya pasaka pamoja na wanafunzi wangu.