Matthew 26:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mnajua kwamba baada ya siku mbili tutakuwa na sikukuu ya Pasaka, na Mwana wa Mtu atatolewa ili asulubiwe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kama mnavyojua, baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, naye Mwana wa Adamu atasalitiwa ili asulubiwe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mnajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa asulibiwe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Mnajua kuwa kesho kutwa ni Pasaka. Siku hiyo Mwana wa Adamu atakabidhiwa kwa maadui zake ili auawe msalabani.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Mnajua kwamba baada ya siku mbili tutakuwa na sikukuu ya Pasaka, na Mwana wa Mtu atatolewa ili asulubiwe.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mnajua kwamba baada ya siku mbili tutakuwa na sikukuu ya Pasaka, na Mwana wa Mtu atatolewa ili asulubiwe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mnajua kwamba baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, naye Mwana wa Adamu atasalitiwa ili asulibiwe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kama mnavyojua, baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, naye Mwana wa Adamu atasalitiwa ili asulubiwe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mnajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa asulubiwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mnajua kwamba baada ya siku mbili tutakuwa na sikukuu ya Pasaka, na Mwana wa Mtu atatolewa ili asulubiwe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmejua, baada ya siku mbili itakuwa Pasaka; naye Mwana wa mtu atatolewa, awambwe msalabani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mnajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa asulibiwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Munajua kwamba kumebaki siku mbili mbele ya kutimia kwa sikukuu ya Pasaka, na Mwana wa Mutu apate kutolewa kusudi atundikwe juu ya musalaba.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa apate kusulibiwa.