Matthew 26:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naam, Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu yasemavyo, lakini ole wake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu. Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwana wa Adamu atakiendea kifo chake kama Maandiko yanavyosema. Lakini ole wake mtu yule anayemsaliti Mwana wa Adamu ili auawe. Ni bora mtu huyo asingezaliwa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naam, Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu yasemavyo, lakini ole wake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naam, Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu yasemavyo, lakini ole wake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwana wa Adamu yu aenda kama alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu. Ingelikuwa bora kwake kama asingelizaliwa!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu. Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naam, Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu yasemavyo, lakini ole wake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwana wa mtu anakwenda njia yake, kama alivyoandikiwa; lakini yule mtu, ambaye Mwana wa mtu atachongewa naye, atapatwa na mambo. Ingalimfalia yule mtu, kama asingalizaliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwana wa Mutu atakufa sawa vile Maandiko Matakatifu yanavyosema juu yake, lakini ole kwa mutu yule atakayemutoa! Ingekuwa heri kwake kama asingezaliwa!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa: lakini ole wake mtu yule ambae Mwana wa Adamu anasalitiwa nae! Ingekuwa kheri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.