Matthew 26:42 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akaenda tena mara ya pili akasali: “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kipite bila mimi kukinywa, basi, utakalo lifanyike.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, basi mapenzi yako yafanyike.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaenda tena mara ya pili, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha Yesu akaenda mara ya pili na akaomba akisema, “Baba yangu, ikiwa ni lazima nikinywee kikombe hiki na haiwezekani nikakwepa, basi mapenzi yako na yatimizwe.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akaenda tena mara ya pili akasali: “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kinipite bila mimi kukinywa, basi, mapenzi yako yafanyike.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akaenda tena mara ya pili akasali: “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kipite bila mimi kukinywa, basi, utakalo lifanyike.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, basi mapenzi yako yafanyike.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, basi mapenzi yako yafanyike.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaenda tena mara ya pili, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniondokee nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akaenda tena mara ya pili akasali: “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kipite bila mimi kukinywa, basi, utakalo lifanyike.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaenda tena mara ya pili, akaomba akisema: Baba, isipowezekana, hiki kinipite, nisikinywe, basi, uyatakayo wewe na yafanyike!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaenda tena mara ya pili, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akawaacha tena kwa mara ya pili, akaomba akisema: “Ee Baba yangu, kama kikombe hiki cha mateso hakiwezi kupita mbali nami, bila mimi kukikunywa, basi mapenzi yako yafanyike!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaenda tena marra ya pili, akaomba, akinena, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kinipitie nisipokinywa, bassi, mapenzi yako yafanyike.