Matthew 26:43 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaja tena, akawakuta wamelala; maana macho yao yamekuwa mazito.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha akarudi na kwenda walipokuwa wafuasi wake, akawakuta wamelala tena. Hawakuweza kukesha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaja tena, akawakuta wamelala; maana macho yao yalijawa na usingizi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokuja tena, akawakuta, wamelala usingizi, kwani macho yao yalikuwa mazito.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaja tena, akawakuta wamelala; maana macho yao yamekuwa mazito.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliporudi tena, akawakuta wanafunzi wale wamelala usingizi, kwa maana macho yao yalikuwa yamewezwa sana na usingizi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaenda, akawakuta wamelala tena; maana macho yao yalikuwa mazito.