Matthew 26:45 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawaambia, “Je, mngali mmelala na kupumzika? Tazameni! Saa yenyewe imefika, na Mwana wa Mtu atatolewa kwa watu wenye dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akarudi kwa wanafunzi wake, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Tazameni, saa imefika ambapo Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akawajia wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike tazama, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dhambi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha Yesu akawarudia wafuasi wake na akasema, “Bado mnalala na kupumzika? Wakati wa Mwana wa Adamu kukabidhiwa kwa wenye dhambi umewadia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawaambia, “Je, mngali mmelala na kupumzika? Tazameni! Saa yenyewe imefika, na Mwana wa Mtu atatolewa kwa watu wenye dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawaambia, “Je, mngali mmelala na kupumzika? Tazameni! Saa yenyewe imefika, na Mwana wa Mtu atatolewa kwa watu wenye dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akarudi kwa wanafunzi wake akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Tazameni, saa imefika ambapo Mwana wa Adamu hana budi kutiwa mikononi mwa wenye dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akarudi kwa wanafunzi wake, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Tazameni, saa imefika ambapo Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akawajia wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike tazama, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawaambia, “Je, mngali mmelala na kupumzika? Tazameni! Saa yenyewe imefika, na Mwana wa Mtu atatolewa kwa watu wenye dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akawajia wanafunzi, akawaambia: Mwafuliza kulala usingizi, uchovu uwatoke? Tazameni, saa iko karibu, Mwana wa mtu atiwe mikononi mwa wakosaji!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akawajia wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike tazama, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akarudi kwenye wanafunzi wake na kuwaambia: “Mungali munalala na kupumzika? Angalia, saa imetimia, sasa Mwana wa Mutu anatolewa katika mikono ya wenye zambi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Khalafu akawaendea wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa hatta mwisho, kapumzikeni: saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dbambi.