Matthew 26:48 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo aliyetaka kumsaliti Yesu, alikuwa amekwisha kuwapa ishara akisema: “Yule nitakayembusu ndiye; mkamateni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yuda aliyekuwa amkabidhi Yesu kwao, alipanga kufanya kitu cha kuwajulisha yupi kati ya wafuasi alikuwa Yesu. Alisema, “Mtu nitakayembusu ndiye mtakayemkamata.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyo aliyetaka kumsaliti Yesu, alikuwa amekwisha wapa ishara akisema: “Yule nitakayembusu ndiye; mkamateni.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo aliyetaka kumsaliti Yesu, alikuwa amekwisha kuwapa ishara akisema: “Yule nitakayembusu ndiye; mkamateni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara kwamba: “yeye nitakayembusu ndiye, mkamateni.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo aliyetaka kumsaliti Yesu, alikuwa amekwisha kuwapa ishara akisema: “Yule nitakayembusu ndiye; mkamateni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mwenye kumchongea alikuwa amewapa kielekezo akisema: Nitakayemnonea ndiye, mkamateni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yuda, yule aliyekuwa amemutoa, aliwapa kitambulisho hiki: “Yule nitakayemubusu ndiye yeye, mumukamate.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na yeye anaemsaliti amewapa ishara, akinena, Nitakaembusu, ndiye; mkamateni.