Matthew 26:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wakasema, “Isiwe wakati wa Sikukuu, kusitokee ghasia miongoni mwa watu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wakasema, Isiwe wakati wa sikukuu, isije ikatokea ghasia katika watu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakasema, “Hatuwezi kumkamata Yesu wakati wa sherehe ya Pasaka. Hatutaki watu wakasirike na kusababisha vurugu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wakasema, “Isiwe wakati wa sikukuu, la sivyo kutakuwa na ghasia miongoni mwa watu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wakasema, “Isiwe wakati wa Sikukuu, kusitokee ghasia miongoni mwa watu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wakasema, Isiwe wakati wa sikukuu, isije ikatokea ghasia miongoni mwa watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini walisema: Kwanza sikukuu ipite, watu wasije, wakafanya fujo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wakasema, Isiwe wakati wa sikukuu, isije ikatokea ghasia katika watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini walijisemesha: “Tusimukamate kwa wakati wa karamu, kusudi fujo isitokee kati ya watu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakanena, Sio wakati wa siku kuu, isije ikatokea ghasia katika watu.