Matthew 26:53 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, hamjui kwamba ningeweza kumwomba Baba yangu naye mara angeniletea zaidi ya vikosi kumi na viwili vya malaika?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, unadhani siwezi kumwomba Baba yangu naye mara moja akaniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakika unajua kuwa ningemwomba Baba yangu yeye angenipa zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, hamjui kwamba ningeweza kumwomba Baba yangu naye mara angeniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, hamjui kwamba ningeweza kumwomba Baba yangu naye mara angeniletea zaidi ya vikosi kumi na viwili vya malaika?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, unadhani siwezi kumwomba Baba yangu naye mara moja akaniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, unadhani siwezi kumwomba Baba yangu naye mara moja akaniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, hamjui kwamba ningeweza kumwomba Baba yangu naye mara angeniletea zaidi ya vikosi kumi na viwili vya malaika?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Au unadhani: Siwezi kumbembeleza Baba yangu, naye akaniletea sasa hivi malaika wengi kupita elfu kumi na mbili?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haujui kwamba ninaweza kumwomba Baba yangu musaada na mara moja angenitumia zaidi ya makundi kumi na mawili ya wamalaika?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu sasa hivi, akaniletea zaidi ya majeshi thenashara ya malaika?