Matthew 26:55 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huohuo Yesu akauambia huo umati wa watu waliokuja kumtia nguvuni, “Je, mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kana kwamba mimi ni mnyanganyi? Kila siku nilikuwa hekaluni nikifundisha, na hamkunikamata!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo, Isa akaambia wale umati wa watu, “Je, mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang’anyi? Siku kwa siku niliketi Hekaluni nikifundisha, mbona hamkunikamata?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka kama kumkamata mnyang'anyi, wenye panga na marungu, ili kunishika? Kila siku naliketi hekaluni nikifundisha, msinikamate.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha Yesu akaliambia kundi, “Kwa nini mnakuja kunikamata mkiwa na mikuki na marungu kama vile mimi ni mhalifu? Nimekuwa nakaa eneo la Hekalu nikifundisha kila siku. Kwa nini hamkunikamata kule?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati huohuo Yesu akauambia huo umati wa watu waliokuja kumtia nguvuni, “Je, mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kama kwamba mimi ni mnyang'anyi? Kila siku nilikuwa Hekaluni nikifundisha, na hamkunikamata!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huohuo Yesu akauambia huo umati wa watu waliokuja kumtia nguvuni, “Je, mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kana kwamba mimi ni mnyang'anyi? Kila siku nilikuwa hekaluni nikifundisha, na hamkunikamata!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo Yesu akawaambia ule umati wa watu, “Mmetoka na panga na marungu kuja kunikamata kama vile mimi ni mnyang'anyi? Siku kwa siku niliketi Hekaluni nikifundisha, mbona hamkunikamata?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo, Isa akawaambia ule umati wa watu, “Je, mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang’anyi? Siku kwa siku niliketi Hekaluni nikifundisha, mbona hamkunikamata?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka kama kumkamata mnyang'anyi, wenye panga na marungu, ili kunishika? Kila siku niliketi hekaluni nikifundisha, msinikamate.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huohuo Yesu akauambia huo umati wa watu waliokuja kumtia nguvuni, “Je, mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kana kwamba mimi ni mnyanganyi? Kila siku nilikuwa hekaluni nikifundisha, na hamkunikamata!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Saa ile Yesu akawaambia yale makundi ya watu: Mmetoka wenye panga na rungu, mnikamate mimi, kama watu wanavyomwendea mnyang'anyi. Kila siku nilikaa hapa Patakatifu nikifundisha, lakini hamkunikamata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka kama kumkamata mnyang’anyi, wenye panga na marungu, ili kunishika? Kila siku naliketi hekaluni nikifundisha, msinikamate.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yesu akawaambia watu wale: “Mumekuja na panga na magongo kwa kunikamata kama watu wanavyokwenda kumukamata munyanganyi? Siku zote niliikaa ndani ya hekalu, nikifundisha, nanyi hamukunikamata.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka, mfano wa watu wafukuzao mnyangʼanyi mna panga na marungu, kunitwaa? Killa siku naliketi mbele zenu hekaluni, nikifundisha, wala hamkunikamata.