Matthew 26:58 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa kuhani mkuu, akaingia ndani pamoja na walinzi ili apate kuona mambo yatakavyokuwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Petro akamfuata kwa mbali hadi uani kwa kuhani mkuu. Akaingia ndani, akaketi pamoja na walinzi ili aone litakalotukia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro alimfuata Yesu lakini alikuwa mbali kidogo. Alimfuata mpaka katika ua wa nyumba ya kuhani mkuu. Petro alienda uani na akakaa pamoja na walinzi. Alitaka kuona nini kingetokea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa Kuhani Mkuu, akaingia ndani pamoja na walinzi ili apate kuona mambo yatakavyokuwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa kuhani mkuu, akaingia ndani pamoja na walinzi ili apate kuona mambo yatakavyokuwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Petro akamfuata kwa mbali mpaka uani kwa Kuhani Mkuu. Akaingia ndani akaketi pamoja na walinzi ili aone litakalotukia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Petro akamfuata kwa mbali hadi uani kwa kuhani mkuu. Akaingia ndani, akaketi pamoja na walinzi ili aone litakalotukia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa kuhani mkuu, akaingia ndani pamoja na walinzi ili apate kuona mambo yatakavyokuwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Petero akamfuata mbalimbali, mpaka akafika uani kwa mtambikaji mkuu, akaingia ndani akakaa pamoja na watumishi, uone mwisho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Petro akamufuata Yesu kwa mbali, hata akaingia ndani ya upango wa Kuhani Mukubwa. Akaingia katika kiwanja, akaikaa pamoja na walinzi kusudi aone mambo yatakayotokea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Petro akamfuata kwa mbali hatta behewa ya kuhani mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.