Matthew 26:65 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, kuhani mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi? Sasa mmesikia kufuru yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo kuhani mkuu akararua mavazi yake na kusema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? Tazama, sasa ninyi mmesikia alivyokufuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kuhani mkuu aliposikia hili, alilarua vazi lake kwa hasira. Akasema, “Mtu huyu amemtukana Mungu! Hatuhitaji mashahidi zaidi. Ninyi nyote mmesikia matusi yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo, Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi? Sasa mmesikia kufuru yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, kuhani mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi? Sasa mmesikia kufuru yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Kuhani Mkuu akararua nguo zake na kusema, “Amekufuru! Kwa nini tunahitaji ushahidi zaidi? Tazama, sasa ninyi mmesikia hayo makufuru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo kuhani mkuu akararua mavazi yake na kusema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? Tazama, sasa ninyi mmesikia hayo makufuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, kuhani mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi? Sasa mmesikia kufuru yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mtambikaji mkuu alipozirarua nguo zake, akasema: Amekwisha kumbeza Mungu. Mashahidi tunawatakia nini tena? Tazameni, sasa hivi mmesikia, anavyombeza Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Kuhani Mukubwa akapasua nguo zake na kusema: “Mutu huyu amemutukana Mungu! Hatuhitaji tena ushuhuda wowote juu yake. Angalia, munatoka kusikia jinsi alivyomutukana Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra kuhani mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru: tuna haja gani ya mashahidi wengine? Sasa mmesikia kufuru yake: