Matthew 26:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya thamani kubwa, alimjia pale mezani alipokuwa amekaa kula chakula, akammiminia hayo marashi kichwani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye mwanamke mmoja akamjia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya thamani kubwa. Akayamimina kichwani mwa Isa alipokuwa ameketi mezani kula chakula.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya thamani kubwa alimkaribia akaimimina kichwani pake alipoketi chakulani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwanamke alimwendea, akiwa na chupa yenye manukato ya thamani kubwa. Yesu akiwa anakula, mwanamke huyo akamwagia manukato hayo kichwani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya thamani kubwa, alimjia pale mezani alipokuwa amekaa kula chakula, akammiminia hayo marashi kichwani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya thamani kubwa, alimjia pale mezani alipokuwa amekaa kula chakula, akammiminia hayo marashi kichwani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mwanamke mmoja alimjia akiwa na chupa ya marumaru yenye manukato ya thamani kubwa, akayamimina kichwani mwa Yesu alipokuwa ameketi mezani kula chakula.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye mwanamke mmoja akamjia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya thamani kubwa; akayamimina kichwani mwa Isa alipokuwa ameketi mezani kula chakula.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya thamani kubwa alimkaribia akaimimina kichwani pake alipoketi chakulani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya thamani kubwa, alimjia pale mezani alipokuwa amekaa kula chakula, akammiminia hayo marashi kichwani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akamjia mwanamke mwenye kichupa cheupe cha jiwe kilichojaa mafuta ya maua yaliyo yenye bei kubwa. Akammiminia kichwani pake, alipokaa akila.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya thamani kubwa alimkaribia akaimimina kichwani pake alipoketi chakulani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mwanamuke mumoja aliingia ndani ya nyumba, akiwa na chupa la jiwe lenye kuwa na marasi ya bei kali, akaimimia juu ya kichwa cha Yesu walipokuwa wakikula.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mwanamke mwenye chombo cha alabastro cha marhamu ya thamani kubwa alimkaribia, akaimimina kichwani pake alipoketi akila.