Matthew 26:73 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye kidogo, watu waliokuwa pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika, wewe pia ni mmoja wao, maana msemo wako unakutambulisha.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya muda mfupi, wale waliokuwa wamesimama pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana usemi wako ni kama wao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Punde kidogo, wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya muda mfupi baadaye, watu waliokuwa wamesimama pale wakamwendea Petro na kumwambia, “Tunajua wewe ni mmoja wao. Hata namna unavyoongea inaonesha wazi kuwa ndivyo hivyo.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baadaye kidogo, watu waliokuwa pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika, wewe pia ni mmoja wao, maana msemo wako unakutambulisha.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye kidogo, watu waliokuwa pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika, wewe pia ni mmoja wao, maana msemo wako unakutambulisha.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya muda mfupi wale waliokuwa wamesimama pale wakamwendea Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana ile namna yako ya kusema ni kama yao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya muda mfupi, wale waliokuwa wamesimama pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana usemi wako ni kama wao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Punde kidogo, wale waliokuwapo wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye kidogo, watu waliokuwa pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika, wewe pia ni mmoja wao, maana msemo wako unakutambulisha.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Punde kidogo wakamjia Petero waliosimama pale, wakamwambia: Kweli, na wewe u mwenzao, kwa maana matamko yako yanakutambulisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Punde kidogo, wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma kidogo, wale waliosimama pale, wakamufikia Petro na kumwambia: “Hakika wewe ni mumoja wao, kwa maana hata usemi wako unakutambulisha.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Punde kidogo, wale waliosimama karibu wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika na wewe u mmoja wao; maana hatta usemi wako wakutambulisha.