Matthew 26:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Ya nini hasara hii?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Upotevu huu wote ni wa nini?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wanafunzi wake walipoona, wakachukiwa, wakasema, Ni wa nini upotevu huu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wanafunzi walipomwona mwanamke akifanya hivi walimkasirikia. Walisema, “Kwa nini kuharibu manukato hayo?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Ya nini hasara hii?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Ya nini hasara hii?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Kwa nini ubadhirifu huu wote?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Upotevu huu wote ni wa nini?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wanafunzi wake walipoona, wakakasirika, wakasema, Ni wa nini upotevu huu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Ya nini hasara hii?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wanafunzi walipoviona wakachukiwa, wakasema: Upotevu huu ni wa nini?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wanafunzi wake walipoona, wakachukiwa, wakasema, Ni wa nini upotevu huu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafunzi wake walipoona jambo lile, wakachukizwa na kusema: “Kwa nini kupoteza mali namna hii?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wanafunzi wake walipoona, wakachukiwa, wakinena, Ya nini upotevu huu?