Matthew 27:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumuua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri pamoja dhidi ya Isa ili kumuua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mapema asubuhi, viongozi wote wa makuhani na viongozi wazee walikutana na kuamua kumwua Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumwua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumuua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri pamoja dhidi ya Yesu ili kumwua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri pamoja dhidi ya Isa ili kumuua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumuua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilipokuwa asubuhi, watambikaji wakuu wote na wazee wa kwao wakamlia Yesu njama, kwamba wamwue.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulipokucha, wakubwa wote wa makuhani na wasimamizi wa watu wakakata shauri la kumwua Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ILIPOKUWA assubuhi, makuhani wakuu wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumfisha;