Matthew 27:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa akamwuliza, “Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamwambia, “Wewe umesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo Isa akiwa amesimama mbele ya mtawala, mtawala akamuuliza, “Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?” Isa akasema, “Wewe wasema hivyo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yesu akasimama mbele ya liwali; liwali akamwuliza, akasema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, Wewe wasema.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alisimama mbele ya Gavana, Pilato, ambaye alimwuliza Yesu, “Wewe ni mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Waweza kusema hivyo.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa akamwuliza, “Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamwambia, “Wewe umesema.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa akamwuliza, “Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamwambia, “Wewe umesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Yesu akiwa amesimama mbele ya mtawala, mtawala akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akasema, “Wewe wasema hivyo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo Isa akiwa amesimama mbele ya mtawala, mtawala akamuuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Isa akasema, “Wewe wasema hivyo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yesu akasimama mbele ya mtawala; mtawala akamwuliza, akasema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, Wewe wasema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa akamwuliza, “Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamwambia, “Wewe umesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu alipopelekwa mbele ya mtawala nchi, mtawala nchi akamwuliza akisema: Wewe ndiwe mfalme wa Wayuda? Yesu akamwambia: Wewe unavyosema, ndivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yesu akasimama mbele ya liwali; liwali akamwuliza, akasema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, Wewe wasema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipopelekwa mbele ya liwali, yeye akamwuliza: “Wewe ndiwe Mufalme wa Wayuda?” Yesu akamujibu: “Wewe umesema.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akasimama mbele ya liwali: liwali akamwuliza, akinena, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, Wewe wanena.