Matthew 27:29 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki wakisema, “Shikamoo mfalme wa Wayahudi!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wakasokota taji la miiba, wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, na wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki, wakisema, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha wakatengeneza taji kutokana na matawi ya miiba na kuiweka kwenye kichwa chake na wakaweka fimbo kwenye mkono wake wa kulia. Kisha kwa kumdhihaki, wakainama mbele zake. Wakasema, “Tunakusalimu, mfalme wa Wayahudi!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki wakisema, “Shikamoo mfalme wa Wayahudi!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki wakisema, “Shikamoo mfalme wa Wayahudi!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakasokota taji ya miiba wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki wakisema “salamu, mfalme wa Wayahudi!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakasokota taji ya miiba, wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, na wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki, wakisema, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakasokota taji la miiba, wakaliweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki wakisema, “Shikamoo mfalme wa Wayahudi!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakasuka kilemba cha miiba, wakamvika kichwani, wakampa mwanzi mkononi mwake mwa kuume, wakampigia magoti, wakamfyoza na kusema: Pongezi, mfalme wa Wayuda!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakasokota taji na tawi lenye miiba na kumuvalisha nalo kwenye kichwa chake. Wakaweka tete katika mukono wake wa kuume, wakapiga magoti mbele yake na kumuchekelea, wakisema: “Jambo, Mufalme wa Wayuda!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na unyasi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamfanyizia dhihaka, wakinena, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!