Matthew 27:35 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokwisha kumsulubisha, wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura. [Hili lilifanyika ili litimie neno lililonenwa na nabii, “Waligawa nguo zangu miongoni mwao na vazi langu wakalipigia kura.”]
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walipokwisha kumsulibisha, waligawa mavazi yake, wakipiga kura; [ili litimie neno lililonenwa na nabii, Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi langu walipiga kura.]
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Askari walimgongomea Yesu msalabani, kisha wakacheza kamari ili wagawane nguo za Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipokwisha kumsulibisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura, [ili litimie lile neno lililonenwa na nabii, “Waligawa nguo zangu miongoni mwao na vazi langu wakalipigia kura.”]
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokwisha kumsulubisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura. [Hili lilifanyika ili litimie lile neno lililonenwa na nabii, “Waligawa nguo zangu miongoni mwao na vazi langu wakalipigia kura.”]
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Walipokwisha kumsulubisha, waligawana mavazi yake, kwa kupiga kura; [ili litimie neno lililonenwa na nabii, Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi langu walipiga kura.]
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokwisha kumwamba msalabani wakazigawanya nguo zake na kuzipigia kura, kusudi yatimie yaliyosemwa na mfumbuaji kwamba: Wakajigawanyia nguo zangu, nalo vazi langu wakalipigia kura.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walipokwisha kumsulibisha, waligawa mavazi yake, wakipiga kura; [ili litimie neno lililonenwa na nabii, Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi langu walipiga kura.]
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao walipokwisha kumutundika juu ya musalaba, wakagawanya nguo zake kwa kuzipigia kura.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Walipokwisha kumsulibi, wakagawa nguo zake, wakipiga kura: illi litimie neno lililonenwa na nabii. Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi langu walipiga kura.