Matthew 27:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akawaambia, “Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe.” Lakini wao wakasema, “Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akasema, “Nimetenda dhambi, kwa maana nimeisaliti damu isiyo na hatia.” Wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakasema, Basi, haya yatupasani sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yuda aliwaambia, “Nimetenda dhambi. Nimemsaliti kwenu mtu asiye na hatia ili auawe.” Viongozi wa Kiyahudi wakajibu, “Hilo halituhusu. Ni tatizo lako, siyo letu sisi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akawaambia, “Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe.” Lakini wao wakasema, “Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akawaambia, “Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe.” Lakini wao wakasema, “Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akasema, “Nimetenda dhambi, kwa maana nimeisaliti damu isiyo na hatia.” Wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akasema, “Nimetenda dhambi, kwa maana nimeisaliti damu isiyo na hatia.” Wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakasema, Basi, haya yatuhusu nini sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akawaambia, “Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe.” Lakini wao wakasema, “Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akisema: Nimekosa nilipotoa mtu asiyepaswa na kumwagwa damu yake. Wale wakasema: Jambo hilo hatumo, litazame mwenyewe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakasema, Basi, haya yatupasani sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akawaambia: “Nimekosa kwa kumutoa mutu huyu asiyekuwa na kosa auawe.” Lakini wao wakamujibu: “Jambo hilo halituelekei. Ni kazi yako wewe mwenyewe!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akinena, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na khatiya. Wakanena, Bassi, haya yatukhussu nini sisi? Tazama wewe hayo.